Masila. Makau

Kuna tofauti gani kati ya VICOBA na SACCOS? (swehemu ya kwanza)

Kuna tofauti gani kati ya VICOBA na SACCOS? (swehemu ya kwanza)VICOBA na SACCOS ni vikundi vya kiuchumi vyote vina malengo sawa isipokuwa mfumo wa uendeshaji.

VICOBA ni kikundi au vikundi vya watu 15 hadi 30 hivi wanaofahamiana ambao wameamua kuunda kikundi ili kupata huduma za mafunzo mbalimbali, huduma za fedha na kuwekeza miradi ya pamoja kwa urahisi na kwa gharama nafuu.

SACCOS                                                                                             

Saccos  ni  asasi  ya  kifedha.Ni  muungano  wa  watu  ambao  lengo  lao  ni  kukusanya  fedha    na  kukopeshana  au  kufanya  biashara  moja  kwa  moja  na kugawana  faida.  

IDADI YA WANACHAMA

Idadi ya wanachama kwenye kikoba ni kati ya watu 15 hadi 30 kwa kila kikundi bali kwenye saccos hakuna kikomo cha idadi ya wanchama.

UONGOZI

Vikundi vya vikoba huwa na viongozi maalum watatu wanaochaguliwa na wanchama ndani ya chama husika nao ni; Mwenyekiti, Makamu Na Mhazini. Bali, Muundo wa Uongozi katika saccos hua ni Bodi au Menejimenti na vyombo hivi huongoza wanachama wote